Noble Quran » Swahili » Sorah At-Takwir ( The Overthrowing )

Choose the reader


Swahili

Sorah At-Takwir ( The Overthrowing ) - Verses Number 29
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ( 1 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 1
Jua litakapo kunjwa,
وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ( 2 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 2
Na nyota zikazimwa,
وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ( 3 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 3
Na milima ikaondolewa,
وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ( 4 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 4
Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ( 5 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 5
Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,
وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ( 6 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 6
Na bahari zikawaka moto,
وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ( 7 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 7
Na nafsi zikaunganishwa,
وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ( 8 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 8
Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ( 9 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 9
Kwa kosa gani aliuliwa?
وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ( 10 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 10
Na madaftari yatakapo enezwa,
وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ( 11 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 11
Na mbingu itapo tanduliwa,
وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ( 12 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 12
Na Jahannamu itapo chochewa,
وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ( 13 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 13
Na Pepo ikasogezwa,
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ( 14 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 14
Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ( 15 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 15
Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ( 16 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 16
Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ( 17 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 17
Na kwa usiku unapo pungua,
وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ( 18 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 18
Na kwa asubuhi inapo pambazuka,
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ( 19 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 19
Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ( 20 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 20
Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ( 21 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 21
Anaye t'iiwa, tena muaminifu.
وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ( 22 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 22
Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.
وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ( 23 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 23
Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ( 24 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 24
Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ( 25 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 25
Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.
فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ( 26 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 26
Basi mnakwenda wapi?
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ( 27 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 27
Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ( 28 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 28
Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ( 29 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Ayaa 29
Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Random Books

Choose language

Choose Sorah

Random Books

Choose tafseer

Participate

Bookmark and Share